Alshabab yasajili wakenya Eastleigh
Huwezi kusikiliza tena

Al-Shabab yasajili wakenya Eastleigh

Kenya inakabiliwa na changamoto mpya za kiusalama katika vita vyake vya kupambana dhidi ya ugaidi.

Al Qaeda inayohusishwa na kundi la Al Shabab hivi karibuni limeanza kuwalenga Wakenya katika mchakato wa kutafuta wapiganaji.

Baadhi ya wapiganaji wapya tayari wamepewa mafunzo Somalia na sasa wamerudi mitaa ya Nairobi.

Mwandishi wa BBC Dennis Okari amekuwa akifanya uchunguzi katika kitongoji cha Eastleigh mjini Nairobi, eneo lenye Wasomali wengi zaidi lijulikanalo kama Mogadishu ndogo ya Kenya.