Papa ahimiza amani katika rasi ya Korea

Haki miliki ya picha AP
Image caption Papa Francis amehimiza mazungumzo baina ya mataifa ya Korea

Papa Francis amezitaka mazungumzo ya amani katika rasi ya Korea.

Papa Francis amesema kuwa hakuna haja ya maonyesho ya nguvu za kijeshi kama ilivyoshuhudiwa leo asubuhi alipotua.

Korea Kaskazini iliporusha makombora baharini muda mchache tu baada ya ke kutoa mjini Seoul.

Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki yuko barani Asia kwa ziara yake ya kwanza tangu kuteuliwa kwake kuwa Papa, Machi 2013.

Katika hotuba iliyomwendea rais wa korea Kusini Park Geun-hye miongoni mwa viongozi wengine papa alisema amani katika rasi ya Korea ndiyo urithi wanaoyopaswa kuwaachia watoto wao.

Wakati wa ziara hii, papa Francis atatoa wakfu kwa waumini wa kanisa katholiki waliofariki kwa Imani yao, na pia atahudhuria tamasha la vijana.

Image caption Papa Francis amezitaka Mazungumzo ya amani katika rasi ya Korea.

Kanisa la katholiki la Korea ya Kusini ni mojawapo ya makanisa yanayokua kwa kasi ulimwenguni.

Kanisa hilo lina waumini milioni tano nukta nne (5.4), asilimia kumi nukta nne (10.4%) ya idadi ya watu nchini humo.

Korea ya Kaskazini ililenga maroketi kwenda pwani ya mashariki mwa Korea ya Kusini, karibu na wakati alipowasili papa.

Aidha Korea ya Kaskazini ilirusha maroketi matatu Alhamisi asubuhi, wakati ambapo ndege aliyokuwa akisafiria papa ilikuwa inakaribia eneo la anga ya Korea ya Kusini.

Pia Korea ya Kaskazini ilirusha maroketi mawili mchana huo, kulingana na mashirika ya habari.

Pyongyang imejishughulisha na kutekeleza mashambulizi kama hayo miezi michache iliyopita, na kudai inajibu machukizo ya Marekani na Korea ya Kusini, huku kero la hivi punde kabisa kwa Korea ya Kaskazini likiwa operesheni

ya kijeshi inayotarajiwa kuanzishwa siku ya Jumatatu.

Rais Park Geun-hye alikuwa katika uwanja wa ndege kumsalimu Papa.

Papa anatarajiwa kuhudhuria sherehe ya kutoa ishara ya heshima kwa baadhi ya wakatholiki wa kwanza wa Korea ya Kusini, atakapotoa wakfu kwa waKorea 124 waliofariki karne ya 18 na ya 19.

Image caption Papa Francis amezitaka Mazungumzo ya amani katika rasi ya Korea.

Baada ya mtu kupewa wakfu mtu hutambulishwa kuwa “aliyebarikiwa,” unapotaja jina lake.

Takriban watu milioni moja wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ya kupewa kwa wakfu itakayofanyika Jumamosi katika bustani ya Gwanghwamun, kati ya mji wa Seoul.

Papa pia atahudhuria siku ya vijana, tamasha ya Kikatholiki katika eneo hilo.

Pia anatarajiwa kukutana na wanafunzi walioponea kifo katika ajali ya feri ya Sewol iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 300.

Ibada ya Amani na maridhiano itafanyika katika kanisa kuu la dayosisi la Myeong-dong Jumatatu, siku ya mwisho ya ziara ya papa.

Kulingana na shirika la habari la Yonhap, kwenye ibada hiyo, Papa atatoa hotuba ya Amani kwa wa-Korea waliogawanyika na pia kwa watu wa Asia ya mashariki.

Korea ya Kaskazini ilipuuza aliko la kanisa la dayosisi ya Seoul la wakatholiki kumi wa Korea ya Kaskazini kuhudhuria ibada ya mwisho, maafisa kutoka Korea ya Kusini wanatuarifu.

Image caption Wakorea wakimshangilia Papa Francis

Idadi ya wakatholiki walioko Korea ya Kaskazini haijabainishwa.

Ripoti ya baraza la haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa iliyotolewa Februari 2014 ilisema, mbali na baadhi ya makanisa yanayothibitiwa na Taifa hilo, wakristu hawaruhusiwi kuwa waumini na wanaokiuka huteswa.

Papa Francis atakuwa Papa wa kwanza kuzuru eneo la Asia kwa kipindi cha miaka 20.

Papa Francis anatarajiwa kuzuru eneo hilo tena Januari mwakani atakaposafiri kwenda Sri Lanka na Ufilipino.

Ufilipino na Timor ya Mashariki ndizo nchi mbili tu zilizo na maumini wengi wa kikatholiki.

Papa John Paul II ndiye alikuwa papa wa mwisho kuzuru Korea ya Kusini mwaka 1989, alipoombea kuungana kwa Korea ya Kaskazini na ya Kusini.

Wakati huo huo, akiwa safarini kwenda Korea ya Kusini, papa pia alituma ujumbe wa simu ya maandishi kwenda kwa viongozi wa China, utamaduni Papa anaposafiri kwa ndege na kupitia juu ya nchi yoyote.

“Nawatakia kila la kheri rais na wananchi wa China, na nawaombea Baraka za mungu za Amani na ustawi katika nchi yenu,” ujumbe huo ulisema.

Vatican haina mahusiano yoyote na Beijing, Beijing haitambui utawala wa Vatican na inaendesha kanisa lake la Katholiki kivyake.

Wakati wa mwisho Papa alizuru eneo hilo, ilimbidi kuepuka eneo la anga ya China.

Lakini katika anchokiita msemaji wa kanisa “ishara ya kulegeza uadui,” ndege aliyosafiria papa iliruhusiwa kupitia eneo la anga la China.

Zaidi ya wa-China 100 walitarajiwa kuhudhuria siku ya vijana wa ki-Asia, lakini karibu 50 kati yao hawakuweza kuhudhuria kwa sababu ya “hali ya utata ndani mwa China,” alisema msemaji wa kamati ya kupanga ziara ya Papa.