Canada itatoa dozi 1,000 kwa WHO

Image caption Canada itatoa dozi 1,000 kwa WHO

Canada imesema itatoa dozi 1,000 za chanjo ya majaribio ya Ebola ili kusaidia kupigana na mlipuko wa ugonjwa huo Afrika magharibi.

Hii ni baada ya shirika la afya duniani WHO kuidhinisha matumizi ya dawa ambazo hazijakamilishwa majaribio ilikuokoa maisha ya watu walioambukizwa Ebola.

Licha ya hayo wataalamu wanasema usambazaji wa dawa hiyo ya Zmapp ni mdogo sana kwani inagharimu muda mrefu kwa wanasayanzi kukuza mimea inayotoa dawa hiyo kwa wingi .

Zaidi ya watu 1,000 wamekufa kutokana na mlipuko huu wa majuzi magharibi mwa Afrika..

Canada inasema kwamba kati ya dozi 800 na 1,000 ya chanjo hiyo ambayo imejaribiwa kwa wanyama tu itatolewa kwa Shirika la Afya ulimwengu kwa matumizi Afrika Magharibi lakini itaweka kifungu kidogo cha chanjo hiyo kwa ajili ya utafiti na ikiwa itajika nchini Canada.

Mlipuko huu umeambukiza watu nchini Guinea, Sierra Leonne, Liberia na Nigeria.

Daktari Gregory Taylor naibu wa Shirika la afya nchini Canada alisema aliona chanjo hizo kama rasilmali ya dunia yote.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Daktari akimtibu mgonjwa wa Ebola Sierra Leone

Aliongezea kusema alikuwa amepewa ushauri kwamba ingekuwa na maana kwa wafanyakazi wa huduma za afya kupewa chanjo hiyo kufuatia uwezekano wao mkubwa wa kupata ugonjwa huo.

Mwanahabari wa BBC aliyeko Toronto Canada anasema kuwa japo Canada itatoa dozi yake nyingi kati ya zilizopo.

Itawachukua muda mrefu wa takriban miezi sita kwa Wataalamu kutengeneza kiwango kikubwa kitakachotosha kuuzuia ugonjwa huu.

Jumanne iliyopita , shirika la afya ulimwenguni WHO lilisema kwamba,kufuatia mlipuko unavyoenea na idadi kubwa ya vifo, ilikuwa sawa kutoa dawa ambazo hazijajaribiwa bado kama matibabu yaliyo na uwezo ama kizuizi cha ugonjwa huu.

Wiki iliyopita, shirika la afya ulimwenguni lilitangaza mlipuko huo wa Ebola kama hatari ya afya kote duniani.

Watu wasiopungua 1,013 wameaga dunia kutokana na kuambukizwa virusi hivyo katika ukanda wa Afrika Magharibi.

Hatua hii ilichukuliwa huku Liberia ikitangaza kuwa ilihitaji kupata dawa la kufanyia majaribio liitwalo Zmapp baada ya kuiomba serikali ya Marekani.

Image caption Canada itatoa dozi 1,000 kwa WHO

Huku hayo yakijiri, serikari ya Liberia imesema kuwa madawa yatakayofanyiwa majaribio yatafikishwa nchini humo baadae juma hili – ingawa watengenezaji wa dawa madawa hayo Mapp Bio pharmaceutical walikuwa wameonya kuwa madawa hayo ni haba.

Zmapp imetumiwa kuwatibu wafanyikazi wawili wa US aid ambao walionyesha dalili ya kupata nafuu.

Padri mmoja wa kanisa la Roman Catholic, aliyeambukizwa virusi vya Ebola nchini Liberia, na ambaye aliaga dunia baada ya kurejea nyumbani kwao nchuni Uhispania pia amedhaniwa kuwa alikuwa amepewa dawa hizo.

Hata hivyo, dawa hizo zimejaribiwa kwa nyani tu na bado haijatathminiwa kuwa ni salama kwa binadamu.

Shirika la afya dunini WHO linasema kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Africa sasa imepita watu 1000.