Uchunguzi Kenya baada ya kushindwa

Image caption Kenya imeanzisha uchunguzi dhidi ya safu ya ukufunzi kufuatia kushindwa na Lesotho.

Shirika la kandanda la Kenya limemsimamisha kazi mkurugenzi wake wa kiufundi Jacob Ghost Mulee.

Mulee ambaye zamani alikuwa ni kocha wa timu ya Harambee stars amefutwa kazi kufuatia uchunguzi unaofanywa kutokana na kushindwa kwa timu ya taifa ya Harambee stars na Lesotho mapema mwezi huu.

Wakati huo huo FKF imempa aliyekuwa kocha wa taifa Adel Amrouche makataa ya saa 48 ( hadi ijumaa) kujieleza kwa nini mkataba wake usisitishwe kwa kuletea taifa aibu baada yake kumtemea mate afisa wa CAF katika mechi dhidi ya Comoros mwezi wa Mei na hatimaye akapigwa marufuku ya mwaka mmoja na shirikisho hilo.

Amrouche alipigwamarufuku ya mwaka mmoja na shirikisho la soka Barani Afrika kufuatia tuhuma hizo dhidi yake.

Image caption Kenya imeanzisha uchunguzi dhidi ya safu ya ukufunzi kufuatia kushindwa na Lesotho.

Hata hivyo Amrouche amekuwa akisisitiza kuwa bado anakandarasi ya miaka mitano na shirikisho la soka la Kenya FKF na kuwa mkataba wake haujakatizwa.

Kulinganan na Taarifa hiyo iliyotolewa na shirikisho la FKF,kamati ya watu saba chini ya uenyekiti wa Profesa Moni Wekesa imeteuliwa kuchunguza kiini cha Kenya kushindwa na Lesotho katika mchujio wa kufuzu kwa dimba la mabingwa barani Afrika.

Kamati hiyo inapaswa kutoa mapendekezo yake baada ya wiki tatu.

Ripoti iliyotiwa sahihi na mkurugenzi mkuu wa FKL Michael Esakwa na kutolewa Alhamisi inasema kushindwa kwa Kenya haukuwa kawaida .

Tabia na mwenendo wa Amrouche aliyesimamiswa na CAF imepelekea utengano baina ya wasaidizi wake kwani wote wawili walitaka kuongoza timu hiyo.

Image caption FKF imeanzisha uchunguzi kufuatia kichapo dhidi ya Lesotho

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa wakuu wa Harambee Stars walipuuza uwezo wa wapinzani wao na kupelekea kudhoofisha matumaini ya waKenya.

Azimio hili lilitolewa baada ya Kenya kushuka katika ngazi ya kimataifa yamchezo huu kutoka namabari 95 hadi 104 huku Lesotho ikipanda zaidi.

Mkuu wa FKF Sam Nyamweya Augosti 3 alifutilia mbali safu ya ukufunzi ya timu ya taifa na timu nyingine kuundwa ikiongozwa na kochi mpya Bobby Williamson aliyeteuliwa.