Wachezaji 10 bora bara ulaya watajwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Robben ni miongoni mwa wachezaji wanaowania taji la mchezaji bora bara Ulaya

Kipa wa Ujerumani na Bayern Munich Manuel Neuer Mshambulizi wa Uholanzi Arjen Robben wamejiunga na mshindi wa tuzo la mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ni miongoni mwa wachezaji wanaowania taji la mchezaji bora barani Ulaya.

Watatu hao walichaguliwa na waandishi wa habari za michezo kufuatia utendakazi wao uwanjani katika msimu wa mwaka wa 2013-2014.

Mshindi atatangazwa rasmi tarehe 28 mwezi huu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Muller ni miongoni mwa wachezaji wanaowania taji la mchezaji bora bara Ulaya

Nuer alikuwa ngao ya mabingwa wapya wa dunia Ujerumani huku Robben akitikisa wavu mara 21 .

Kwa upande wake mchezaji bora duniani mwaka huu Christiano Ronaldo alifunga mabao 17 msimu huu na kuiongoza Real Madrid Kutwaa taji la mabingwa barani Ulaya.

Mshindi atatuzwa katika hafla ya kutangaza droo ya mwaka huu ya kuwania kombe la mabingwa barani Ulaya huko Monaco.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Costa ni miongoni mwa wachezaji wanaowania taji la mchezaji bora bara Ulaya

Wachezaji kumi waliteuliwa kulingana na wingi wa pointi waliozojizolea .

Wengine katika Orodha hiyo ni Thomas Muller (Bayern Munich, ) 39 ; Philipp Lahm (Bayern Munich, ) 24, Lionel Messi (Barcelona, Argentina) 24; James Rodriguez (Monaco/Real Madrid, Colombia) 16; Luis Suarez (Liverpool/Barcelona, Uruguay) 13; Angel Di Maria (Real Madrid, Argentina) 12; Diego Costa (Atletico Madrid/Chelsea, Uhispania ) 8.