Gaza yajadiliwa Cairo

Haki miliki ya picha n
Image caption Mazungumzo ya amani yafanyika kumaliza mapigano Gaza

Kiongozi wa ujumbe wa Wapalestina walioko katika mazungumzo ya amani huko Cairo amesema usitishaji mapigano huko Gaza unaweza kuendelea kwa siku tano zaidi.

Maamuzi hayo yamefikiwa ikiwa imesalia karibia saa moja tu kuisha kwa muda wa saa 72 wa usitishaji mapigano kuisha. Afisa wa Palestina Azzam al-Ahmad amesema kumekuwa na maendeleo mazuri wakati wa mazungumzo ya amani yanayosimamiwa na Misri.

Lakini hakuna taarifa yoyote kutoka upande wa Israel zaidi ya kuwa kulikuwa na shambulizi la roketi kutoka Gaza na hivyo kusababisha wapiganaji wa Israel kulipiza kwa kutumia mashambulizi manne ya anga.

Hata hivyo wapiganaji wa Kipalestina wamekanusha kuhusika na mashambulizi ya awali.