Ukraine hamkani si shwari,mjini Donetsk

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Askari akipita karibu na kifaru mjini Donetsk.

Mapigano makali yamezuka katika kitovu cha mji wa Donetsk mashariki mwa Ukraine, na kugharimu maisha ya mtu mmoja na kusababisha majeruhi kadhaa.

Vikosi vya kijeshi vya waasi huko Ukraine vimepiga kambi katika mji huo wa Donetsk na kushambulia vikosi vya serikali,wakati vikosi vya waasi vikinijinasibu hivyo, upande wa serikali wamejigamba kuwatimulia mbali waasi hao nje ya mji huo wa Donetsk.

Na hii si mara ya kwanza mapigano hayo makali kuripuka katikati mwa mji huo wa Donetsk,lakini mapigano hayo ya hivi karibuni yanaelezwa kuwa ni mabaya kuwahi kutokea na yanaelezwa kufika katika hoteli za kifahari pamoja na majengo ya ofisi za serikali na haijulikani nani anamshambulia nani.

Nalo shirika la kutetea haki za binadamu limeyashambulia makundi hayo mawili kwa kuwashambulia raia wasio na hatia,na kufuatia mapigano hayo majeruhi wanaongezeka kila dakika ya mapigano hayo,nao umoja wa mataifa umetoa takwimu ya vifo vilivyosababishwa na mapigano hayo kua ni zaidi ya elfu mbili kwa wiki mbili zilizopita.