Marekani kutumia njia mbadala Iraq

Haki miliki ya picha
Image caption Marekani kutumia njia mbadala kuokoa Wayazidi

Marekani sasa imesema inafikiria kutumia njia mbadala za kuwaokoa maelfu ya Wayazidi, wananchi wa Iraq waliokwama katika mlima kaskazini mwa Iraq wakikimbia kushambuliwa na wapiganaji wa dola ya

Kiislamu.

Ikulu ya Marekani imerudia kauli yake kuwa haitatumia majeshi ya ardhini kupambana na wapiganaji hao wa dola ya kiislam lakini ikasema inaweza kuwatumia katika kutoa msaada wa kibinadamu.

Msemaji wa Ikulu ya marekani Ben Rhodes amesema Serikali yake ilikuwa ikijadili wazo la Ufaransa, Australia na Canada nao kutoa msaada wa kibinadamu.

Kwa upande wa Uingereza Waziri Mkuu David Cameron amesema mipango thabiti ilikuwa ikiwekwa sawa kwa ajili jumuia ya kimataifa kuwaokoa Yazidi.