Mbabe wa vita mbioni nchini Somalia

Image caption 10 walifariki katika mapigano yaliyozuka baada ya wanajeshi kushambulia makazi ya Dai

Mapiganao makali yamezuka katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Hi ni baada ya vikosi vya serikali kuzindua oparesheni leo alfajiri dhidi ya nyumba moja inayomilikiwa na m'babe mmoja wa kivita kama kampeni ya vikosi hivyo kuwapokonya silaha wapiganaji.

Maafisa wanasema kuwa takriban watu kumi waliuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika vita hivyo ,vinavyoonekana kuwa vibaya zaidi tangu wapiganaji wa Al-Shabaab wafurushwe katika mji huo miaka mitatu iliopita.

Vikosi vya serikali vinasema kuwa vimeiteka nyumba hiyo ya Ahmed Dai katika oparesheni iliochukua zaidi ya saa tano.

Ahmed Dai alifanikiwa kutoroka,lakini wapiganaji kadhaa wa kundi lake walikamatwa na silaha zao kuchukuliwa.

Ameambia BBC kwamba ametoroka baada ya wanajeshi wa serikali kuanzisha operesheni kali dhidi yake na wapiganaji wake.

Ahmed Dai huongoza kikosi kikubwa cha wpaiganaji ambao muda wote hutoa ulinzi wa wageni.

Hata hivyo amesema kuwa ataendelea kupigana na kwamba alitumia silaha hizo kujilinda.

Wapiganaji wake walikuwa wakitekeleza oparesheni zao karibu na eneo la uwanja wa ndege linalolindwa sana.

Oparesheni hiyo ya kuwapokonya wapiganaji silkaha ilianza wiki iliopita na serikali inasema kuwa imefanikiwa kupata bunduki 500 pamoja risasi.

Takwimu zinasema kuwa kuna zaidi ya bunduki nusu millioni katika mikono ya raia nchini somali ambako ssheria hazifuatwi