Ebola:IOC yazuia wachezaji wa Afrika

Haki miliki ya picha
Image caption IOC yazuia wachezaji kutoka mataifa yaliyoathirika na Ebola kushirki mashindano ya Vijana China

Wanariadha wanaotokea mataifa yaliyoathirika na homa ya Ebola wamezuia kushiriki makala ya mwaka huu ya mashindano ya olimpiki ya vijana yaliyoanza leo katika mji wa Nanjing Uchina.

Kamati andalizi ya mashindano hayo iliamua kuwatenga wanariadha watatu kutoka Guinea na Nigeria kutoshiriki mashindano ya uogeleaji na yale yanayohusu kugusana .

Kamati ya olimpiliki duniani IOC ilisema kuwa ni vigumu kuenezwa kwa homa hiyo ya Ebola japo wanachukua tahadhari hiyo kwa maslahi ya washiriki wengine.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption IOC yazuia wachezaji kutoka mataifa yaliyoathirika na Ebola kushirki mashindano ya Vijana China

Wanaridha waliohusika na wawili kutoka Guinea na mmoja kutoka Nigeria.

Wanariadha wote hata hivyo watafanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Wanariadha kutoka Sierra Leone ana Liberia waliamua kutosafiri kwenda China.

Mashindano hayo yaliyoanza leo yataendelea hadi tarehe 28 Agosti.