Wachimba migodi wakumbuka Marikana

Marikana, Afrika Kusini Haki miliki ya picha Reuters

Maelfu ya wachimba migodi wa Afrika Kusini wamekusanyika katika mgodi wa dhahabu nyeupe wa Marikana nje ya Johannesburg kukumbuka mwaka wa pili tangu wenzao 34 kuuliwa na polisi.

Viongozi kadha wa upinzani piya walikuwamo katika mkusanyiko huo.

Rais Jacob Zuma alisema hii iwe siku ya kutafakari.

Uchunguzi unaofanywa na wanasheria kuhusu mauaji hayo bado unaendelea.

Jumatatu, naibu rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, alitokeza mbele ya tume hiyo.

Bwana Ramaphosa alikuwamo kwenye bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Lonmin wakati wa mauaji hayo.