Upinzani wamtaka Nawaz Shariff kujiuzulu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Imran Khan na wafuasi wake

Mwanasiasa mashahuri wa upinzani nchini Pakistan Imran Khan amemtaka waziri mkuu Nawaz Shariff Kujiuzulu akimshtumu kwa kufanya udanganyifu wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake katika mji mkuu wa Islamabad ,bwana Khan amesema kuwa wataandamana katika barabara kuu za mji huo hadi pale kiongozi huyo atakapojiuzulu.

Kiongozi mwengine wa Upinzani Tahir-Ul-Qadri anatarajiwa kutoa hotuba kama hiyo baadaye hii leo.

Viongozi hao wawili waliongoza maandamano kutoka mji wa mashariki wa Lahore.

Serikali imesema kuwa iko tayari kuchunguza madai ya udanganyifu ,lakini bwana Sharrif hawezi kuondolewa kupitia mkutano wa hadhara.

Waandishi wanasema kwa maandamano hayo ni changamoto kubwa kwa serikali ya mwaka mmoja ya bwana Shariff.