UN:Wanaowafadhili wapiganaji mashakani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mawaziri wanaoukutana Mjini Brussels kujadili mgogoro wa Iraq

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa pamoja limeamua kuwawekea vikwazo watu binafsi wanaowasajili,kuwafadhili na kuwahami wapiganaji walio na hisia kali.

Waandishi wanasema kuwa uamuzi huo ulioandaliwa na Uingereza unalenga kulidhoofisha kundi la Islamic State nchini Iraq na Syria.

Uingereza inaamini kwamba kundi hilo linategemea ufadhli kutoka nje.

Azimio hilo imewataja watu sita watakaopigwa marufuku kusafiri, huku mali yao ikipigwa tanji mbali na kuwekewa vikwazo vya kununua silaha.

Mmoja ya wale waliotajwa ni msemaji wa kundi hilo la Islamic State.

Uamuzi huo pia unatoa wito kwa makundi yanayoshirikiana na Al Qaeda kusalimu silaha na kuvunjiliwa mbali.