Netanyahu:Usalama wa Israel uzingatiwe

Haki miliki ya picha
Image caption Benjamin Natenyahu

Waziri mkuu nchini Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa hakutakuwa na makubaliano ya kusitishwa vita kwa mda mrefu hadi pale mahitaji ya usalama wa Israel yatakapozingatiwa.

Wajumbe wanaowakilisha Israel na Palestina wanakutana katika mji mkuu wa Cairo nchini Misri ili kuendelea na mazungumzo yao yasio ya moja kwa moja kutafuta mwafaka wa kusitisha vita katika eneo la Gaza.

Netanyahu ameliambia baraza la mawaziri kwamba ujumbe wa Israel katika mazungumzo hayo una jukumu la kuwa na msimamo mkali kuhusu mahitaji hayo ya kiusalama.

Kundi la wapiganaji wa Hamas linataka Israel na Misri kuondoa vikwazo vya mipakani dhidi ya Gaza huku Israel ikilitaka kundi la Hamas kusalimu silaha zao.