Wana Jihad wawauwa watu 700 Syria

Haki miliki ya picha n
Image caption Wapiganaji wa Islamic State

Shirika linalochunguza maswala ya kibinaadamu nchin Syria lenye makao yake nchini Uingereza limesema kuwa wapiganaji wa Islamic state wamewaua watu 700 wa kabila moja mashariki mwa Syria katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Shirika hilo limesema kuwa wengi wa waathiriwa wanatoka katika kabila la al-Sheitaat katika mkoa wa Deir al-Zor ambapo raia waliuawa bila kupewa mda wa kujitetea.

Waandishi wanasema pande hizo mbili zilianza kupigana katika jimbo moja lenye utajiri wa mafuta baada ya kutofautiana .

Awali ,rais wa muungano wa upinzani nchini Syria Hadi Al Bahra alitoa wito kwa ulimwengu kuingilia kati nchini Syria ili kukabiliana na tishio la wanamgambo wa Islamic state.

Mchanganuzi wa BBC katika eneo la mashariki ya kati amesema kuwa serikali ya Syria mara chache hushambulia kambi za Islamic State hatua iliosababisha wapiganaji hao kujiimarisha ikilinganishwa na makundi mengine ya waasi.