Mmarekani mweusi auawa Missouri

Haki miliki ya picha
Image caption waandamanaji St Louis

Mauaji mengine ya raia wa kiafrika yaliyofanywa na polisi katika eneo la St Louis yameongeza hali ya wasiwasi na vurugu katika eneo hilo ambalo kwa takriban siku 11 sasa kumekuwa na vurugu kutokana na mauaji yaliyotokea awali.

Jumanne wiki hii afisa mmoja wa polisi alimpiga risasi na kumuua raia wa kiafrika aliyedaiwa kuwatishia kwa kisu polisi.

Mkuu wa polisi wa St Louis Sam Dotson amesema mauaji hayo ya August 9 ya Michael Brown yameongeza hali ya machafuko katika eneo hilo.

Mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder anatarajiwa kutembelea eneo la Ferguson jumatano wiki hii ili kujadili taaerifa rasmi za uchunguzi wa mauaji hayo.

Mwendesha mashitaka katika kesi ya mauaji ya ya Michael Brown leo amewasilisha ushahidi dhidi ya afisa anayedaiwa kuhusika katika mauaji ya Michael Brown.

Vurugu zimeendelea katika mji huo huku waandamanaji wanaopinga mauaji hayo wakiwa wamepakaa maziwa usoni kujikinga na mabomu ya machozi kufuatia waandamaji wawili kuathirika na mabomu hayo.