Shtuma kufuatia mauaji ya mwandishi

Image caption Picha kutoka kwa kanda hiyo ya video ya James kabla ya kuuawa

Kumekuwa na shutuma za kimataIfa kufuatia kuuawa ukatili kwa mwandishi wa habari raia wa Marekani na kundi la islamic state nchini Syria.

Waziri wa masuala ya kigeni wa Uingereza Philip Hammond amesema kuwa mashirika ya kijasusi yanajaribu kumtambua yule aliyemuua Foley ambaye anaoneka kuwa na lafudhi ya Uingereza.

Rais wa Marekani Barack anatarajiwa kutoa taarifa yake baadaye leo.

Kikosi cha wapiganaji wa kiislam wenye msimamo mkali Islamic State kimeachilia video inayoonesha mauaji ya mwandishi habari mwenye asili ya Marekani aliyetekwa nyara nchini Syria 2012.

Naye waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesitisha mapuziko yake na anarejea mji London .

James Foley alipotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria yapata miaka miwili iliyopita.

Mamake mwandishi huyo ambaye aliuawa na wapiganaji wa jimbo linalodhibitiwa na wapiganaji wa kiislamu nchini Syria, ametoa risala za rambirambi kwa kijana wake na kusema kuwa alipoteza maisha yake akijaribu kufichua dhuluma walizokuwa wakipitia watu wa Syria.

Katika video hiyo mwandishi huyo wa kujitegemea anaonekana kuuawa na mtu anayemruhusu kutoa semi yake ya mwisho.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption James Foley enzi za uhai wake akiwa na vitendea kazi vyake.

Foley ambaye katika video hiyo amevalia magwanda ya rangi ya chungwa akiwa amepiga magoti anasikika akisema kuwa ''Ninawaomba ndugu jamaa na marafiki wangu wasimame na kuzuia adui wangu Serikali ya Marekani kwa ukatili wanaoendelea kutekeleza ndani ya Iraq.''

Mpiganaji mmoja wa kundi hilo akizungumza kwa kizungu anailaumu Marekani kwa kifo cha mwandishi habari huyo.

''Kila siku mnaposhambulia jamhuri ya kiislamu manadhuru maisha ya muislamu na hivyo tunachukua maisha yetu ili iwe onyo kwako (rais) Obama''

anasikika akisema kabla ya kutekeleza kitendo hicho cha kikatali.

Punde baada ya kukamilisha hotuba yake bwana huyo anaanza kumchinja Foley lakini video hiyo inazimwa .

Sekunde chache baadaye mwaandishi mwengine pia raiya wa Marekani Steven Sotloff, anaonekana kabla ya ilani kutolewa kuwa hatima yake iko mikononi mwa Obama na hatua atakayochukua .

Scotloff alitekwa mwaka wa 2013 nchini Syria karibu na mpaka wa Uturuki.

Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley auawe.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption James akiwa kazini.

Katika mtandao wa kijamii wa Facebook familia ya mwandishi huyo iliandika kuwa ’tunajua kwamba wengi wenu mnasubiri uthibitisho ama majibu ya maswali yenu,tafadhalini muwe watulivu mpaka nasi sote tupate taarifa tunazo tamia,na tunaomba muendelee kumbumbuka Foleys na kumwombea kila siku.’’

Katika video hiyo iliyobeba ujumbe unaosomeka kua ujumbe kwa Marekani,mwandishi huyo pia alionekana akiwa chini ya ulinzi wa mtu aliyekua amevalia kinyago usoni,askari huyo alikua akizungumza ndani ya lafidhi yenye athari za Uingereza,akisema kua kifo cha mwandishi huyo ni matokeo ya mashambulizi ya mabomu yanayowalenga wa Iraq.