Wakimbizi wengi Afrika wako Ethiopia

Image caption Wakimbizi wengi Afrika wako Ethiopia.

Ethiopia ndilo taifa linalowahifadhi wakimbizi wengi zaidi barani Afrika.

Kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR Ethiopia inazaidi ya wakimbizi 630,000 .

Kenya inawahifadhi zaidi ya wakimbizi 575,000 asili mia kubwa ikiwa wakimbizi kutoka Somalia na sasa Sudan Kusini.

Takwimu hiyo imetolewa Ethiopia holds a ministerial meeting of six countries that are sheltering Somali refugees…

Msemaji mmoja wa UNHCR Adrian Edwards anasema ongezeko hilo la idadi ya wakimbizi nchini Ethiopia linatokana na mzozo unaoendelea nchini Sudanm Kusini.

Raia wa Eritrea na Somali wanachangia pia idadi hiyo kubwa.

Takwimu za hivi punde kutoka Shirika hilo la Wakimbizi zinasema hadi kufikia sasa, Zaidi ya watu milioni moja nukta nane wamefurushwa makwao kutokana na mzozo huo ulioibuka December mwaka jana.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakimbizi wengi Afrika wako Ethiopia.

Kati ya idadi hiyo, takriban laki mbili unusu wamekimbilia Ethiopia.

Hii imepelekea Kambi nyingi za wakimbizi kufunguliwa katika kipindi cha miezi michache iliyopita.

Edwards ameonya kuwa msimu wa mvua ulioanza umefanya maisha ya wakimbizi katika kambi nyingi za Umoja wa Mataifa kuwa ngumu zaidi.

Wakati huohuo, shirika la misaada la Care International limeonya kuwa jamii ya kimataifa inaendelea klujivuta katika kutoa fedha za msaada kwa raia wa Sudan Kusini, licha ya hali mbaya nchini humo.

Mratibu wa shuguli za dharura wa Care International Caroline Saint-Mleux anasema licha ya jamii ya kimataifa kuahidi mwezi Mei kutoa dola bilioni moja nukta nane kwa ajili ya Sudan Kusini, kiwango hicho bado hakijafikiwa.