Amani ya Gaza ni muhimu

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amesema kwamba hatapumzika katika kutafuta suluhu ya amani na kuondoa vikosi vya askari huko Gaza ,mpaka hapo amani ya ukanda wa Gaza itakapopatikana.

Netanyahu aliyasema hayo alipokua akizungumza kwa njia ya Television,na hakusita kuvizungumzia vikosi vya kijeshi vya Palestina na hasa Hamas vilivyoko Syria vilivyo chini ya itikadi ya dini ya kiislam ambavyo viko Syria na hata Iraq.

Kikundi cha Hamas kimeshafanya uharibifu mkubwa kwa kurusha maelfu ya maroketi kuelekea Israel katika kipindi cha ukiukwaji mkubwa wa amri ya kusitisha mapigano kwa siku kumi

Israel nayo inalaumiwa kwa kuvurumusha maroketi kuelekea ukanda wa Gaza.Kundi la Hamas limedai kwamba mkuu wao wa majeshi Mohammed Deif,alinusurika kwenye makombora mapema wiki hii,katika jaribio la kutaka kumuangamiza.

Wakati Deif ananusurika katika jaribio hilo, mke na mwanawe wa kiume hawakusalimika waliuawa mara moja, na inasemekana maelfu ya waombolezaji walijitoma katika mitaa ya Gaza kwenda kushiriki maziko hayo,huku wakijiapiza kulipiza kisasi baadaye.