Wapiganaji wa Kurdi washikilia Monsul

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption wapiganaji wa Kikurdi

Wapiganaji wa Ki Kurdi waliopo kaskazini mwa iraq wamesema kuwa kwa sasa wanadhibiti eneo lote la bwawa la Mosul baada ya kulikomboa kutoka kwa wapiganaji wa Kiislam kwa mapigano ya siku mbili mfululizo.

Mwandishi wa BBC aliyepo katika bwawa hilo anasema amesikia milio ya risasi na milipuko eneo karibu kabisa na Wakurdi ambapo jeshi la Iraq linaendelea kuklabiliana na wapiganaji hao wa Kiislam ili kuwaondoa katika eneo hilo.

Hata hivyo kusini mwa Iraqi pia majeshi ya serikali yameendelea kupambana na makundi ya wapiganaji wa Kishia ili kuukomboa mji wa Tikrit unaokaliwa na wapiganaji hao japo kuwa inadaiwa kuwa wanakabiliwa na upinzani mkali..