Wahanga ndege ya Malaysia waibiwa fedha

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ndege ya shirika la ndege ya malaysia wakati wa uhai wake.

Ofisa mmoja mwanamke mwenye cheo cha juu katika bank kubwa iliyoko mjini Kuala Lumpur , Malaysia pamoja na mumewe wameshtakiwa kwa kuiba mamilioni ya dola za kimarekani kutoka katika account za abiria na wafanyakazi wa ndege iliyopotea ya Malaysia Air Line MH370 ambayo ilipotea katika mazingira ya kutatanisha,katika bahari ya Hindi mapema mwezi March.

Pamoja na kushtakiwa huko, mtu na mkewe hao waliepuka makosa mengine yapatayo 16 kati ya makosa hayo yamo wizi,kukaidi amri ya mahakama na makosa mengineyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mke na mumewe washtakiwa kwa wizi wa pesa za marehemu

Ofisa huyo Nur Shila Kanan anatuhumiwa kutumia cheo chake vibaya katika benki ya HSBC nchini Malaysia kwa kupoka pesa.

Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama moja mjini Kuala Lumpur,Malaysia kwamba wawili hao walifanikiwa kukwapua dola za kimarekani elfu thelathini kutoka katika account tatu tofauti za abiria waliopotea na account moja ni ya mfanyakazi wa shirika hilo la Malaysia Air Line.