Ebola:Polisi wavunja maandamano Liberia

Haki miliki ya picha a
Image caption Maafisa wa usalama wakiwa Westpoint baada ya uvamizi wa kituo cha Ebola

Polisi nchini Liberia wamerusha vitoa machozi kuwatawanya umati uliojaa hasiria katika mji mkuu Monrovia wakipinga kuzingirwa kwa kitongoji chao na maafisa wa Usalama.

Maafisa wa usalama walilazimika kutumia nguvu baada ya waandamanaji kuanza kuwapura kwa mawe katika kitongoji cha Westpoint .

Awali rais Ellen Johnson Sirleaf alikuwa ametangaza hali ya tahadhari na amri ya kutotoka nje kwa wenyeji wa vitongoji hivyo vilivyoathirika na ugonjwa wa Ebola.

uliokuwa ukiandamana kupinga kuzingirwa kwa eneo wanakoishi kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa ebola

Walioshuhudia walisema kuwa vikosi vya usalama vilivyotumwa kuzuia kutembea kwa watu baada ya kituo cha afya kuvamiwa wiki iliyopita viliwaudhi watu ambao walijipata hawana tena uhuru wa kutoka maeneo hayo ya Westpoint.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahudumu wa Afya wakipuliza dawa ya kuzuia kuenea kwa Ebola

Rais Sirleaf alikuwa ametangaza amri ya kutotoka nje nyakati za usiku kuanzia saa tatu hadi saa kum na mbili asubuhi.

kufuatia amri hiyo Watu hawakuruhusiwa kuingia au kutoka nje ya eneo la kitongoji cha West Point viungani mwa jiji la Monrovia.

Aidha, eneo fulani katika mji mkuu wa Monrovia litatengwa katika harakati za kuthibiti kuenea kwa ugonjwa hatari wa Ebola.

Watu waliojawa na hamaki walishambulia kituo cha afya katika eneo la West Point siku ya Jumamosi, na kupelekea kutoroka kwa wagonjwa 17 wa Ebola.

Rais Sirleaf amelaumu serikali yake kwa kutothibiti homa hiyo ya Ebola, kwani haikufanya vya kutosha kuboresha hali ya maisha ya raia walipopuuza ushauri wa wafanyakazi wa huduma za afya na kutotilia maanani tahadhari rasmi za Ebola.

Hata baada ya Liberia kutangaza hali ya dharura kufuatia mlipuko wa Ebola mapema mwezi huu, ugonjwa huo unazidi kusababisha vifo nchini humo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf atangaza amri ya kutotoka nje .

Ebola haina tiba lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) liliidhinisha matumizi ya dawa zilizokuwa zikifanyiwa utafiti kufuatia mlipuko mkubwa wa Ebola Afrika Magharibi .

Kwa mujibu wa waziri wa maswala ya habari wa Liberia, Lewis Brown, madaktari watatu walioambukizwa Ebola wakiwahudumia wagonjwa wa Ebola, wameonyesha dalili za kuimarika kiafya, baada ya kutumia dawa zilizokuwa zikifanyiwa majaribio juma lililopita.

Watu 1,229 wameripotiwa kufarika katika kanda ya Magharibi mwa Afrika tangu ugonjwa huo uzuke miezi minne iliyopita.

Ebola husambazwa moja kwa moja kupitia maji maji ya mwili ya waliougua .