Ramsey atolewa kwa kadi ya njano

Haki miliki ya picha PA
Image caption Aaron Ramsey

Mchezaji Ramsey jana amejikuta matatani baada ya kutolewa nje ya uwanja kutokana na kupewa kadi ya pili ya njano katika michuano hiyo ya mabingwa barani Ulaya wakati timu yake ya Arsenal ilipokwaana na Besiktas.

Hata hivyo mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Demba Ba aliwashtua Arsenal pale alipoachia mkwaju mkali toka umbali mrefu uliogonga mwamba.

Matokeo mengine ni Copenhagen kubamizwa mabao 3 kwa 2 dhidi ya Leverkusen,Salburg ikaibwaga Malmo bao 2 -1, Napol na Anthletic Bilbao wakitoa sare ya 1-1.

Naye mshambuliaji mpya wa Real Madrid James Rodriguez ameweza kujipatia goli la kwanza tangu avae jezi za klabu.