Africa kusini yafunga Mipaka yake

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kila mtu kwao kwa usalama wetu sote.

Nchi ya Africa Kusini inafunga mipaka yake kwa wasafiri kutoka katika nchi za Liberia,Guine na Sierra Leone nchi hizo tatu zimeathiriwa vibaya na mripuko wa ugonjwa wa Ebola

Waziri wa Afya wa taifa hilo, Aaron Motsoaledi,amesema kwamba marufuku hiyo haiwahusu raia wa nchi hiyo ingawa watalazimika kukaguliwa kitabibu ili kubaini endapo watakuwa wamepata uambukizo.

Nao Umoja wa Africa umesema kwamba utaunda timu madhubuti ambayo ni maalumu kwa nchi hizo nne kutoka Africa Magharibi zilizoathiriwa na ugonjwa huo.timu hiyo itahusisha watabibu watakao shirikiana na watabibu wa nchi husika katika kuutokomeza ugonjwa huu.

Pengine haya ni matunda ya ukosoaji wa madaktari wasio na mipaka kuukosoa umoja huo wa mataifa kwa kushindwa kuwajibika kuhusiana na ugonjwa huo.