Mtetezi wa Haki za Binaadamu aaga Dunia

Ulimwengu wa watetezi wa haki za binadamu leo umo katika msiba mzito kufuatia kifo cha mwanzilishi wa harakati hizo Helen Bamber kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 89.

Hellen alianza harakati zake kwa kuwasaidia watu waliokua wameteswa katika vita vya kwanza vya dunia mnamo mwaka 1945, alipokua akifanya kazi na manusura wa mauaji ya kutisha ya Nazi .

Utetezi wake kwa binaadamu waliokosa haki zao umedumu kwa kipindi cha miaka 70 akihamasisha kutetea haki za binaadamu na ndipo mwaka 2005, akazindua the Helen Bamber Foundation.

Mrs Bamber, alizaliwa kaskazini mwa mji wa London mnamo mwaka 1925 akiwa ni chotara kiizrael na Poland .