India :Utafiti wafutilia mbali Ubakaji

Haki miliki ya picha n
Image caption India :Utafiti wafutilia mbali Ubakaji

Uchunguzi uliofanyika kwa nguo za wasichana watatu waliouliwa na kusemakana kubakwa umebaini kuwa hawakubakwa .

Wasichana hawa walipatikana wakining'inia kwenye mti kijijini Uttar Pradesh mwezi Mei jambo ambalo lilikasirisha ulimwengu.

Washukiwa watatu na polisi wawili walikamatwa kufuatia tukio hilo.

Kwa wakati huo,uchunguzi huo ulionyesha walibakwa mara kadhaa kabla ya vifo vyao kutakana na kutiwa kitanzi.

Mwanzoni kesi hiyo ilifanyiwa uchunguzi na polisi wa humo kabla yao kuwapisha wachunguzi wa India.

Haijulikani vile matokeo hayo yasiofanana yatashughulikiwa

Mwezi uliopita wachunguzi kutoka Shirika la ujasusi la India CBI walijaribu kufukua miili ya wasichana hao bila mafanikio kwani makaburi hayo yalikuwa yamefurika na hadi kufikia sasa haijawezekana kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha .

Mmsemaji wa CBI alieleza chombo cha habari cha BBC kuwa iliwabidi watumie nguo zao ambazo hazikuwa na ushahidi wowote .

Ushahidi wa mwanaume pia haukupatikana

Habari hii ya kuuwawa kwa wasichana hawa inaendelea kuwa mbaya kila uchao huku waliowekwa kizuizini wakiendelea kukaa gerezani miezi tatu tangu kisa hicho.

Haki miliki ya picha n
Image caption Visa vya Ubakaji vimeenea India

Hivi karibuni ripoti za uchunguzi wa India umeleta utata kwenye taarifa hiyo na kupelekea waliotoa ushahidi kushukiwa.

Wazazi wa walioadhirika walisema kuwa polisi walichukua zaidi ya saa 12 kuchukua hatua kwa ripoti kuwa wasichana hao walikuwa wametoweka.

Wanasemekana kuwa na umri wa 14 NA 15 na walitoweka walipokuwa wameenda choo kwani nyumbani kwao hamkuwa na choo na kupatikana siku iliyo fuatia.

Visa vya kudhulumiwa kimapenzi nchini India vimeongezeka tangu ubakaji wa wingi uliotokea 2012 na kuuliwa kwa mwanafunzi akiwa katika basi la Delhi ,hivyo kupelekea serikali kukaza sheria kwa wabakaji.

This case also sparked a debate about the dangers for rural women who have to travel to nearby fields in order to use the toilet.

Msemaji wa idara ya upelelezi nchini India ameambia BBC kuwa matokeo ya karibuni yaliyofanyiwa katika lebu ya kisasa katika mji wa Hyderebad, yanaonyesha kuwa wasichana hao wawili ambao ni mabinamu hawakubakwa.

Haki miliki ya picha n
Image caption Mauaji ya wasichana hao yaliibua hasira duniani.

Wasichana hao ambao walikuwa wa hadhi ya chini katika Jamii ya Wahindi, walitoweka baada ya kutoka nyumba usiku wakienda kutumia choo kilicho nje ya nyumba.

Walipatikana wakininginia juu ya mti siku iliyofuata na uchunguzi wa awali ulionyeshwa kuwa walibakwa na genge la wanaume.

Wanaume watatu walikamatwa kuhusiana na uhalifu huo pamoja na maafisa wawili wa polisi ambao walilaumiwa kwa kujaribu kuficha uhalifu wa washukiwa.

Kesi hiyo ilizusha hasira kubwa miongoni mwa raia wa India katika taifa ambalo lilikuwa limeshuhudia matukio mengi ya magenge kuwabaka wanawake.

Maafisa wa polisi sasa wameanza kuchunguza iwapo mauaji ya wasichana hao yanatokana na mauaji yanayofanywa na baadhi ya jamii nchini humo kwa watu wanaodhania kuwa wasichana wameawaaibisha kwa kushiriki mapenzi na watu wa hadhi ya chini.