Waziri mkuu wa Israel alionya Hamas

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Benjamin Netanyahu

Waziri mkuu nchini Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa kundi la wapiganaji wa Hamas litagharamika vibaya kufuatia mauaji ya kijana mmoja wa miaka minne aliyeuawa na shambulizi la roketi kutoka Gaza.

Netanyahu ameliagiza jeshi lake kuimarisha mashamblizi dhidi ya wapiganaji wa kipalestina katika eneo la Gaza.

Kijana huyo ni raia wanne wa Israel na mtoto wa kwanza kuuawa katika mgogoro huo.

Zaidi ya raia 2000 wa Palestina wakiwemo watoto 400 wamefariki tangu vita hivyo vizuke mnamo mwezi Julai.

Mapema siku ya ijumaa wanamgambo wa kipalestina waliwauwa watu 18 wanaoshukiwa kuwa wapelelezi wa Israel.