Malori ya msaada yarudi Urusi.

Image caption Malori ya misaada ya Urusi

Malori yote ya msafara wa misaada kutoka Urusi ambayo yalisafiri bila idhini hadi katika eneo linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa Ukraine siku ya ijumaa yamerudi nchini Urusi.

Afisa mmoja wa forodha amesema kuwa malori kadhaa yalikaguliwa na kurudi nchini Urusi.

Zaidi ya malori mia mbili ya misaada yalisafiri hadi katika mji wa Luhansk siku ya ijumaa,baada ya Urusi kusema kuwa imechoka kungojea idhini kutoka kwa serikali ya Ukraine.

Urusi inasema kuwa msaada huo ulikuwa wa kibinaadamu,lakini mataifa ya Magharibi yanasema kuwa unatumiwa na Urusi kuvamia Ukraine.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kufanya mazungumzo mjini Kiev na rais wa Ukraine Petro Poroshenko pamoja na waziri mkuu Arseniy Yatsenyuk.