WHO:Itachukua mda kukabili Ebola

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ebola

Shirika la afya duniani WHO limeonya kuwa ueneeaji wa haraka wa Ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika si jambo la kawaida na kwamba itachukua miezi kadhaa ili kuudhibiti ugonjwa huo.

limeonya kuwa viwango vya ugonjwa huo vilipuuzwa kwa sababu nyingi ikiwemo ile ya familia kuwaficha wagonjwa katika majumba yao.

Shirika hilo pia limesema kuwa kuna maeneo ambayo maafisa wa matibabu hawawezi kufika.

Kufikia sasa zaidi ya vifo 1400 vimethibitishwa nchini Liberia,Guinea,Sierra leone na Nigeria.