Mchezaji afariki baada ya kupigwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mechi

Mchezaji mmoja wa soka raia wa Cameroon amefariki baada ya kupigwa na kitu katika kichwa chake kilichorushwa kutoka kwa mashabiki mwishoni mwa mechi katika ligi ya Algeria.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 Albert Ebosse aliyekuwa akiichezea kilabu kubwa ya JS Kabylie alikuwa ameifungia timu yake bao la pekee katika mechi ambayo timu hiyo ilishindwa kwa mabao mawili kwa moja na kilabu ya USM Alger.

Kitu kilichomgonga kichwani kilirushwa baada ya mechi kukamilika,wakati ambapo wachezaji walikuwa wanarudi katika chumba cha kujianda.

Waziri wa maswala ya ndani nchini Algeria ameagiza kuanzishwa uchunguzi kuhusu mauaji hayo.