Ukraine:Urusi inapanga msafara mwengine

Image caption Msafara wa msaada ulipoingia Ukraine juma lililopita

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema Urusi inapania kupeleka msaada zaidi Ukraine kwani hali ya kibinadamu inazidi kuzorota.

Ukraine haikuruhusu msafara wa msaada wa kwanza na kupelekea utata mpakani maafisa wa Kiev walipowanyima kibali cha kuingia Ukraine bila kukaguliwa.

Wakati huo Kiev Ilikuwa ikielezea wasiwasi wake kuwa Moscow ilikuwa iwapo silaha kuwepo kwa silaha .

Viongozi wa Ukraine walisema msafara wa magari yaliokuwa na silaha yalivuka mpaka wake kutoka Urusi jumatatu na kupelekea mapigano.

Image caption Viongozi wa Ukraine na Urusi wanaratibiwa kukutana Kesho

Mfara huo unasemekana ulikuwa karibu na Mariupol kusini mashariki mwa Ukrain .

Zaidi ya watu 2000 wamekufa na wengine 33000 kuhamishwa makwao katika miezi kadhaa iliyopita kwenye mapigano kati ya serikali ya Ukraine na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.

Rais wa Urusi na Ukraine wamepanga kukutana katika mji wa Minski Belatus jumanne ili kuzungumzia swala hilo.

Bwana Lavrov alieleza kuwa alikuwa ametuma ujumbe kwa waziri wa mambo ya kigeni wa Ukraine kumjulisha kuhusu msafara mpya uliotarajiwa.

Aidha alitaka makaubaliano ya kufikikisha msaada wa pili kwa njia ile ile siku ya awali.

Ukraine ilisema magari karibu 30 yalikuwa yameingia kutoka Urusi karibu na Mariupol mnamo jumatatu ikiwa na alama ya waasi wa jimbo linalotaka kujitenga la kidemokrasia ya Donetsk

Haki miliki ya picha AP
Image caption Urusi imepanga msafara mpya wa msaada kwenda mashariki mwa Ukriane

Bwana Larvov alisema kuwa wako tayari kwa suluhu lolote maadamu matokeo yaonekane akiongeza kuwa Urusi ilitaka kuwasaiida Ukraini kuleta uwiano baina yao.

Vurugu mashariki mwa Ukraini ilitokea mwezi Aprili ambapo walitangaza kutaka kujitenga na Ukraine katika maeneo ya Donetsk na Luhask .