Afghanistan:Abdullah asusia hesabu ya kura

Image caption Wawakilishi wa Abdulah wanadai udanganyifu unaendelea

Waendeshaji kampeni za mojawapo wa wagombea urais nchini Afghanistan Abdullah Abdullah wamesusia ukaguzi wa kura leo, wakisema matakwa yao ya kusitisha udanganyifu hayajatimizwa.

Ukaguzi kamili wa kura hizo zilizopigwa kumtafuta atakayemrithi rais Hamid Karzai umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Umoja wa mataifa unajitayarisha kuimarisha hatua za kuzuia udanganyifu kwa kutuma waangalizi zaidi kuhakikisha kwamba shughuli ya kuhesabu tena kura hizo unakamilika.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Shughuli ya Ukaguzi wa Kura umeendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja

Maafisa nchini Afghanistan chini ya usimamizi wa Umoja wa mataifa wanaendelea na shughuli ya kuchosha ya kuhesabu upya kura kuhakikisha kuwa kuna usawa katika uchauzi huo.

Lakini wakati ukaguzi wa kura hizo ulipoingia awamu yake ya mwisho wiki hii, huku maboxi kadhaa pekee ndiyo yaliotupwa, kundi la Abdullah wamesema watasusia shughuli hiyo.

Linaamini kwamba malefu ya kura zilipigwa katika duru ya pili ya uchaguzi hu kwa mgoombea aliyeongoza katika uchaguzi huo unaokumbwa na mzozo wa hesabu ya kura, Ashraf Ghani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Viongozi wanaowania Urais nchini Afghanistan walipokutana na Jonh Kerry

Maafisa wa Umoja wa mataifa jana walifanya mikutano usiku na pande zote kuendeleza shughuli hiyo na ni wazi kuwa shughuili hiyo itaendelea wakiwepo au wasipokuwepo waangalizi wa Dr Abdullah.

Huu unaonekana kama wakati hatari mno kaika nchi ambayo madaraka yamebadilika miongoni mwa watu kwa kutishiwa kwa mtutu wa bunduki.

Baadhi ya wafuasi wa Abdullah wametishia kufanya maandamano barabarani iwapo shughui hiyo ya kuheabu upya kura haitofanyika kwa usawa.