Waasi wakana kutungua ndege ya UN

Haki miliki ya picha afp
Image caption Waasi nchini Sudan wamekanusha madai kuwa walktungua helikopta moja ya Umoja wa Mataifa, katika mji wa Bentiu

Vikosi vya waasi nchini Sudan vimekanusha madai kuwa vilidungua helikopta moja ya Umoja wa Mataifa, katika mji wa Bentiu, iliyoko katika jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta wa Unity.

Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini inasema rubani na wahudumu wengine wawili walifariki na mwingine akiponea kifo, ndege hiyo ya mizigo ilipoanguka.

Emmanuel Igunza na mengi zaidi

Saa chache tuu baada ya helikopta hiyo aina ya M1-8 kuanguka, msemaji wa jeshi nchini Sudan Kusini, Kanali Philip Aguer aliwalaumu waasi.

Lakini katika taarifa, msemaji wa waasi hao amekanusha madai hayo kama yasiyokuwa na msingi.

Aidha wametaka uchunguzi wa kina kufanywa kubaini chanzo cha helikopta hiyo kuanguka.

Image caption Waasi wakana kutungua ndege ya UNmjini Bentiu

Tayari umoja wa mataifa umeanzisha uchunguzi wake kuhusu tukio hilo.

Bentiu ni mojawapo ya miji iliyoathirika pakubwa na miezi kadhaa ya mapigano na imebadilishana mikono mara kadhaa tangu mapigano kuanza mwezi Desemba mwaka jana.

Maelfu ya watu wamefariki na wengine zaidi ya milioni moja nukta nane kufurushwa makwao.

Jumatatu wiki hii, pande zote mbili zinazopigana zilitia saini mkataba wa kuimarisha azimio la kumaliza mapigano nchini humo.

Aidha zimepewa makataa ya siku arobaine na tano kubuni serikali ya mpito.