Mashirika hatimaye yafika Gaza

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watoa misaada Gaza

Makundi ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu na shirika la chakula la umoja wa mataifa WFP kwa mara ya kwanza wamevuka mipaka na kuingia ukanda wa Gaza.

taarifa kutoka katika shirika hilo zinasema kuwa waliweza kuingia kwa urahisi kupitia njia ya Rafah ambayo imefunguliwa kwa sharti maalum siku moja baada ya makubaliano kati ya kundi la Hamas na Israel .

Msemaji wa shirika hilo amesema ilikuwa ni muhimu kuingia ukanda wa Gaza kupitia njia tofauti ili kuhakikisha misaada ya kibinadamu inawafikia wahanga wa vita katika eneo hilo.

hata hivyo shughuli za uvuvi bado zimezuiwa pamoja na makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa wiki kadhaa hadi sasa.