Tayyip Erdogan kuapishwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Tayyip Erdogan Rais mteule wa Uturuki akiwapungia mkono wafuasi wake.

Rais mteule wa Uturuki Tayyip Erdogan,anakaribia kuapishwa kufuatia ushindi wa kishindo alioupata katika historia ya nchi hiyo, kwenye uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Erdogan, amekwisha itumiakia ikulu ya Uturuki katika kipindi awamu tatu kama Waziri mkuu,anakaribia kuapishwa na hivyo kutwaa madaraka kama rais mteule.

Nao wadadisi wa mambo nchi Uturuki wanamuelezea Erdogan kipindi hiki cha mpito kitamuongezea uwezo wa uongozi kiongozi huyo.

Sherehe za kuapishwa kwa Tayyip Erdogan kutashuhudiwa na viongozi mashuhuri wa nchi hiyo,Marekani,na pia kutoka katika nchi za Magharibi ambao wametuma wawakilishi kwenye sherehe hizo.

Mwandishi wa habari wa BBC kutoka Ankara anaelezea kushuka kwa mahusiano mema kati ya nchi ya Uturuki na serikali za nchi za Magharibi katika miaka iliyopita ya utawala wa Edorgan .