Urusi yaingilia kati vita ya Ukraine.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kombora likiwa limetua barabarani.

Balozi wa Marekani nchini Ukraine,Geoffrey Pyatt, amesema vikosi vya wanajeshi wa Urusi wanaingilia kati mapigano yanayoendelea kusini mashariki mwa Ukraine.

Geoffrey akiandika katika ukurasa wake wa twitter ameelezea kua vikosi vipya vya Ukraine vimesambazwa vikiwa na zana mpya za kivita ikiwemo makombora ya SA-22. Pyatt alifikia kutoa maelezo yake kufuatia mapigano mapya yaliyozuka katika pwani ya kusini mashariki mwa nchi hiyo na kuarifiwa kua wamekamata eneo lililokua likishikiliwa na vikosi vya Russia katika mji wa Novoazovsk.

Mapema wiki hii kansela wa ujerumani Angela Merkel,alitaka maelezo ya kina kutoka kwa raisi wa Urusi Vladimir Putin kuhusiana na mashambulizi hayo mapya.

Kila wakati, inadaiwa kwamba Urusi imekua ikikana madai kwamba inawapa silaha na kuwaunga mkono waasi .