Meya wa Toronto azua kituko

Haki miliki ya picha AP
Image caption Meya Rob Ford akiwa katika moja ya shughuli zake

Madai mapya yameibuka yakimkabili meya wa mji wa Toronto mwenye vibweka lukuki Rob Ford,ambaye anawania ridhaa ya wananchi wa Toronto mnamo mwezi wa kumi mwaka huu amezua mambo mapya miezi mitatu kabla ya uchaguzi.

madai hayo ya bodi ya shule ya kikatoliki yanadai ,kua Ford aliwalazimisha wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya shule hiyo kujigaragaza kwenye vinyesi vya wanyama,kumtisha mwalimu na inaelezwa kua meya huyo alikua amelewa wakati alipokua akishiriki kwenye mchezo wa mpira wa miguu kama kocha shuleni hapo.

Ikumbukwe kwamba meya Ford alitimuliwa nafasi ya ukocha mwaka wa jana,kufuatia madai hayo kampeni meneja wake aliyaita madai ya shule hiyo kama ni uzushi mtupu.

Kama hiyo haitoshi,Ford alivuta vyombo vya habari na ulimwengu kwa ujumla kwa kukiri hadharani kwamba yeye anatumia dawa za kulevya.