Ebola:Liberia kufunguwa mtaa uliotengwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption KIjiji cha West Point mjini Monrovia ,Liberia

Liberia imesema kuwa itafungua mtaa mmoja wa mabanda uliokuwa umetengwa ili kuukabili ugonjwa wa Ebola.

Waziri wa habari amesema kuwa serikali inaufungua mtaa huo wa West Point,ikiwa na matumaini ya kukabiliana na ugonjwa huo vilivyo.

Mtaa huo uliopo katika mji mkuu wa Monrovia ulitengwa zaidi ya wiki moja iliopita na kusababisha ghasia.

Nchini Senegal mamlaka imethibitisha kisa cha kwanza cha Ebola na kulifanya kuwa taifa la tano magharibi mwa afrika kuathiriwa na ugonjwa huo.

Serikali inasema kuwa virusi vya ugonjwa huo vilipatikana na mtu mmoja kutoka nchi jirani ya Guinea.

Wakati huohuo wanasayansi wanasema kuwa majaribio ya dawa ya Ebola ya Zee-Mapp yameonyesha kuwa dawa hiyo ina uwezo wa asilimia 100 baada ya kujaribiwa katika tumbiri 18 katika maabara.

Hatahivyo uwezo wake miongoni mwa binaadamu haujulikani.

Watu saba wametibiwa na dawa hiyo lakini wawili kati yao waliaga dunia.