AMISOM yashambulia kusini mwa Somali.

Image caption Maafisa wa jeshi la AMISOM

Maafisa wa serikali ya Somali wanasema kuwa vikosi vyao vikishirikiana na wanajeshi wa Amisom wameanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Alshabaab kusini mwa taifa hilo.

Lengo lao ni kuliteka jimbo la Lower Shabelle ambalo linajulikana kwa kuwa ngome kuu ya wapiganaji hao.

Gavana wa jimbo la Lower Shabelle Abdukadir Mohamed Nur amesema kuwa vikosi vya serikali vinapiga hatua kubwa katika oparesheni hiyo ilioanza siku ya ijumaa.