P.M:Tishio la ugaidi Uingereza ni kubwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron

Serikali ya Uingereza inasema kuwa matukio yanayoshuhudiwa nchini Iraq na Syria yameongeza tishio la kufanyika kwa mashambulizi ya kigaidi nchini Uingereza.

Kiwango cha tishio hilo kimeongezeka kutoka kuwa kikubwa hadi kibaya zaidi,ikimaanisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa shambulizi kama hilo ijapokuwa halitafanyika katika siku za hivi karibuni.

Waziri Mkuu David Cameron amesema kuwa kundi la Islamic State ni tishio kubwa kwa usalama wa Uingereza zaidi ya kundi jingine lolote hapo awali.

Tangu kuzinduliwa kwa mfumo mpya wa kuwatahadharisha raia mnamo mwaka 2006,Uingereza imekuwa ikitishiwa na shambulizi la kigaidi kwa takriban miaka minne kwa jumla na tishio hili ni la tatu kwa ukubwa.