Askari wa UN Syria washambuliwa

Askari wa wa kuweka amani wa UN nchini Syria

Serikali ya Philippines inasema kuwa askari wake kama 70 katika kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa nchini Syria, wameshambuliwa na wapiganaji.

Waziri wa Ulinzi wa Philippines, Voltaire Gazmin, alisema wapiganaji walishambulia kambi moja ya Umoja wa Mataifa na askari wa Philippines wameondoshwa katika kambi nyengine.

Msemaji wa jeshi alisema askari hao wako salama.

Siku ya Alkhamisi wapiganaji wa Syria waliwateka askari wa usalama 44 kutoka Fiji katika kambi yao kwenye mlima wa Golan, na walizingira kambi mbili zinazotumiwa na askari kutoka Filippines ambao walikataa kusalimisha silaha zao kwa wapiganaji.

Umoja wa Mataifa umelaani hatua iliyochukuliwa na wapiganaji.

Umoja wa Mataifa unasimamia makubaliano ya mwaka wa 1974 ya kuacha mapigano baina ya Syria na Israel.