Zimapp yazidi kuongeza matumaini

Image caption wiliam

Ndugu wa jamaa Muingereza wa kwanza kukumbwa na ugonjwa wa Ebola tangu ugonjwa huo uzuke huko Africa Magharibi anaendelea vyema.

William Pooley, mwenye umri wa miaka 29, wiki iliyopita alikua bado amewekwa karantini katika hospitali ya Royal Free Hospital mjini London.

Nduguze Robin na Jackie,wamesema wanaelewa jamaa yao anaendelea vyema baada ya kua ‘’bacon butty" na kuusifu uongozi wa hospitali alikolazwa kwa huduma nzuri walizompatia .

Mpaka sasa watu 1,500 wamekwishakufa kutokana na ugonjwa huo tangu uliporipuka kwa mara ya kwanza huko Guinea.

Pooley alikua kwenye kazi ya kujitolea kama muuguzi huko Sierra Leone na ndipo alipoambukizwa ,baada ya kupata ugonjwa huo hakuwaambia jamaa zake,mpaka alipopata uhakika kua ameambukizwa na atarejeshwa nyumbani.

Mamake mzazi aitwaye Jaque alipata taarifa za kuugua kwa mwanawe alipokua kwenye harusi ya ndugu yao,tena walikua katikati ya sherehe na picha zikipigwa, na wakahisi anataka kumtakia mema binamu yake kwa harusi yake.,na babake aitwaye Robin ndiye aliyegundua mwanawe ana matatizo kwa jinsi anavyozungumza .