Iran wahimizwa matumizi ya mitandao

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Hassan Rouhan Iran

Raisi wa Irani,Hassan Rouhan,amewataka wananchi wake pamoja na masheikh kujifunza zaidi masuala ya mitandao ya kijamii, internet na hasa matumizi ya teknolojia mpya (teknohama).

Rouhan alikua akitoa hotuba iliyokua ikirushwa live na runinga ya nchi hiyo,amewaambia wananchi wake kua matumizi ya mtandao yanawaunganisha na ulimwengu wa sayansi,na amewataka vijana pia kuacha kupuuzia matumizi ya mtandao na badala yake wajishirikishe na kuitumia mitandao.

Rais Rouhan alichaguliwa mwaka uliopita,ameahidi kushirikiana nakuwapa uhuru vyombo vya habari nchini mwake,lakini katika mwito huo amekumbana na msimamo mkali wa baadhi ya mashekhe nchini humo.