Marekani yaombwa isaidie Ukraine

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Robert Menendez

Mkuu wa baraza la kamati ya mahusiano ya Marekani ameiomba nchi yake kupeleka silaha Ukraine ili kukabiliana na kinachodaiwa uvamizi unaofanywa na Urusi.

Robert Menendez amesisitiza Umoja wa Ulaya kutoa silaha za kivita kuisaidia Ukraine ili iweze kujihami dhidi ua Urusi.

Wito huo umekuja huku Rais Putin wa Urusi akiita majadiliano ya haraka kuhusiana na mwa Ukraine kama nafasi ya kufanya makubaliano ya kusitisha uhasama wao.

Kauli ya Putin inakuja ikiwa ni siku moja kabla ya mazungumzo yatakayofanyika huko Minsk kati ya Ukraine na Urusi kujadili machafuko hayo.