Watu maarufu waanikwa mitandaoni ulaya

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jennifer Lawrence

Idara ya upelelezi ya nchini marekani FBI linachunguza kwa ukaribu madai ya maelfu ya accounts za watu maarufu kutekwa,na kinachotafutwa hasa ni picha za utupu za watu hao maarufu ambazo zimekua zikianikwa mitandaoni bila ya muwekaji kujulikana.

Hili limemkuta mshindi wa tuzo ya Oscar Jennifer Lawrence ambaye picha zake ziliachiliwa mtandaoni,kampuni ya utengenezaji wa simu za mkononi Apple wamesema wao wanachunguza ikiwa uvujaji wa picha hizo umesababishwa na iCloud.

Apple inasema inachunguza ikiwa akaunti za iCloud zimevamiwa.

Bi Lawrence, ambaye anaigiza katika filamu ya Hunger Games ameomba uchunguzi ufanywe baada ya picha za waigizaji, nyingi zikiwa za uchi kupatikana katika simu za mkononi za waigizaji mashuhuri.