Watu maarufu waanikwa mitandaoni

Haki miliki ya picha Getty
Image caption muathirika wa mitandao Jennifer Lawrence.

Idara ya upelelezi ya nchini marekani FBI linachunguza kwa ukaribu madai ya maelfu ya accounts za watu maarufu kutekwa,na kinachotafutwa hasa ni picha za utupu za watu hao maarufu ambazo zimekua zikianikwa mitandaoni bila ya muwekaji kujulikana.

Hili limemkuta mshindi wa tuzo ya Oscar Jennifer Lawrence ambaye picha zake liachiliwa mtandaoni, kampuni ya utengenezaji wa simu za mkononi Apple wamesema wao wanachunguza ikiwa uvujaji wa picha hizo umesababishwa na iCloud .