Ujerumani kuwapa Wakurd silaha

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeshi la kikurdi nchini Iraq likisherehekea ushindi dhidi ya wapiganaji

Ujerumani inatarajia kulitumia jeshi la Wakurd wa Iraq silaha ikiwemo bunduki na silaha zile zenye mfumo unaoweza kukabiliana na mashambulizi ya vifaru vya kivita.

Jeshi hilo limekuwa likipambana na wapiganaji wa kiislamu kaskazini mwa Iraq.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula Von der Leyen amesema silaha hizo zotaweza kuwatosheleza wanajeshi elfu nne ifikapo mwishoni mwa Septemba.

Amesema uamuzi huo ni kutokana na maslahi ya nchi yake.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na Ujerumani imeelezwa kuwa ni ya nadra sana kwa nchi hiyo, kupeleka silaha kwenye eneo lenye mapigano.

Hata hivyo uamuzi huo umekosolewa na baadhi ya watu ambao wana wasiwasi zitakapoishia silaha hizo.