Saratani ya ngozi: Tishio Uingereza

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Matukio ya ugonjwa wa saratani ya ngozi nchini Uingereza kwa sasa ni mara tano zaidi ya ilivyokuwa katika miaka ya 1970.

Hospitali nchini Uingereza zimeshuhudia ongezeko la wagonjwa wanaolazwa kutokana na tatizo la saratani ya ngozi kwa karibu theluthi ya wagonjwa waliolazwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, takwimu rasmi zimeonyesha.

Wataalam wanasema kuwepo kwa unafuu wa gharama za malipo kwa likizo nchi za nje na mtindo wa kubadili rangi ya ngozi kwa njia ya jua ni mambo ambayo yanatajwa kusababisha ongezeko la magonjwa ya saratani ya ngozi.

Mtaalam wa magoinjwa ya ngozi Dokta Walayat Hussain ameiambia BBC kuwa Uingereza inakabiliwa na "tsunami ya saratani ya ngozi"