Kutakatisha fedha ni haramu

Image caption Bernie Madoff

Mtoto wa mfanyabiashara haramu wa kutakatisha fedha nchini Marekani amefariki dunia.

Andrew Madoff,aliyekua na umri wa miaka 48,alikua akisumbuliwa na maradhi ya kansa.kakake Andrew aliyekua akiitwa,Mark yeye aliamua kujiua miaka takribani minne sasa.

Inaarifiwa kua vijana wote wawili Mark na Andrew walikua wameajiriawa na baba yao aitwaye Bernie,ingawa wote kwa pamoja wakati wa uhai wao walikana kujihusisha na biashara za baba yao na hawakuwahi kukamatwa.

Bernie Madoff anatumikia kifungo cha miaka mia moja na hamsini jela kwa udanganyifu.