Waziri Mkuu wa Lesotho arejea nyumbani

Haki miliki ya picha
Image caption Jeshi la Lesotho lilidaiwa kupanga njama ya kumpindua waziri mkuu Thomas Thabane

Waziri mkuu wa Lesoto Thomas Thabane amewasili nchini mwake baada ya jaribio la kutaka kumpindua.

Bwana Thabane alikimbilia Afrika Kusini siku ya Jumamosi saa chache baada ya wanajeshi kukaribia ikulu yake na kudhibiti vituo vya polisi.

Ripoti zinasema kuwa polisi wa Afrika Kusini kwa sasa ndio wanalinda nyumba za waziri mkuu huyo na naibu wake

Thabane (70) aliwasili Lesotho saa 6 mchana nchini Lesotho na leo viongozi wa vyama vyote 3 vinavyo unda serikali ya mseto ya Lesotho vinatarajiwa kukutana na mfalme wa nchi hiyo Letsie kumuarifu yaliojiri J3 A-Kusini kwenye mkutano wao waku upatanishi ulioongozwa na rais Jacob Zuma.

Haki miliki ya picha
Image caption Waziri mkuu Thomas Thabane

Suala la kulifungua tena bunge la Lesotho lilofungwa na waziri mkuu tangu mwezi Juni ni miongoni mwa mada zitakazo wasilishwa mbele ya mfalme Letsie na shirika la maendeleo la nchi za kusini mwa Afrika SADC ambalo lilimtaka waziri mkuu na naibu wake Metsing walifungue bunge hilo mwezi huu.

Kwa sasa hali ya utulivu inaonekana kuwepo katika mjii mkuu wa Maseru huku Askari polisi wa A-Kusini wakilinda makazi ya waziri mkuu na naibu wake .

Badhi ya repoti zinasema endapo bunge la Lesotho litafunguliwa tena huenda waziri mkuu Dr Thomas Tabane akapigiwa kura ya kutokua na imani nae .